Wizara yatoa maagizo Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi (VETA) Morogoro

NA MWANDISHI WyEST

NAIBU Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga (Mb) ameutaka uongozi wa Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi (VETA) Morogoro kuhakikisha ujenzi wa mabweni kwa ajili ya wanafunzi chuoni hapo unamalizika ifikapo Septemba Mosi,mwaka huu.




Mhe. Kipanga ameyasema hayo alipotembelea chuoni hapo kukagua maendeleo ya ujenzi huo ulioanza mapema mwezi Februari.

Ujenzi wa mabweni hayo ya kisasa umegharimu kiasi cha Shilingi milioni 400 na ulitarajiwa kukamilika Juni 3, hivyo Naibu Waziri amemtaka mkandarasi (Arusha Technical College) kuzingatia maelekezo ya kukamilisha ujenzi huo ndani ya siku 15.



“Mmefanya kazi nzuri lakini bado mpo taratibu ‘speed’ ni ndogo. Hatutaki kila tukija hapa tunaona bado mpo tu, tunataka ifikapo Septemba mosi mumkabidhi Mkuu wa Chuo funguo zake na tuanze maandalizi ya uzinduzi rasmi, ”amesema Kipanga.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Chuo hicho, Samweli Kaali amesema hadi sasa ujenzi wa mabweni hayo umefikia asilimia 95.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news