Watanzania kunogesha maonesho makubwa ya Kiafrika barani Ulaya kuanzia Septemba 1 hadi 4,2022

NA ZAINABU HAMISI

YALE maonesho makubwa ya Kiafrika barani Ulaya (15 International Africa Expo Festival Tuebingen 2022, Germany) yanatarajiwa kuanza mwanzoni mwezi Septemba 1 hadi Septemba 4, 2022 katika viwanja vya Fest Platz,mjini Tuebingen nchini Ujerumani.
Onesho hilo mwanzo lilikuwa lifanyike mwezi huu wa Agosti 2022, lakini likahairishwa kutokana na mashariti ya idadi ya waudhuriaji ambayo yaliwekwa na Halmashauri ya Mji wa Tubingen ambapo mkurugenzi wa onesho hilo, Dkt.Susan Tatah hakuyakubali mashariti hayo.

Aidha,baada ya makubaliano ya mhandaaji na Serikali ya Halmashauri ya Tubingen, kuruhusu idadi ya maelfu ya watu kuudhuria sasa onesho hilo litafanyika mwanzoni mwa mwezi Sepetemba ambapo wageni kutoka kila kona ya Dunia wanatarajiwa kuudhuria.
Pia wajasiriamali wa bidhaa mbalimbali za kiafrika na wasanii wa sanaa mbalimbali za maonesho kutoka kila kona ya Afrika wanatarajiwa kushiriki,zikiwemo taasisi na asasi zisizokuwa za kiserikali nazo zitakuwapo mjini Tubingen,Ujerumani.

Miongoni mwa watakaonogesha maonesho hayo ni mwanamitindo mbunifu wa mitindo rafiki wa mazingira DIANA JOHN MAGESA ambaye mara nyingi amewahi kuipeperusha bendera ya Tanzania katika maonesho ya Kimataifa kama vile New York Fashion Week, African Fashion Week Canada, UNESCO nchini Ufaransa.

Aidha,wasanii wa sanaa za maonesho na wajasiriamali mbalimbali kutoka moja kwa moja nchini Tanzania wanatarajia kuonesha kazi zao katika maonesho hayo nchini Ujerumani.

Post a Comment

0 Comments