Waziri Balozi Mulamula awasili Ubalozi wa Tanzania nchini Congo DR

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akisalimiana na Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Balozi Said Juma Mshana wakati akiwasili katika Ubalozi wa Tanzania -Kinshasa, DRC.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akisaini katika kitabu cha Wageni katika Ubalozi wa Tanzania nchini DRC mara baada ya kuwasili katika ubalozi huo.
Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo DRC kushiriki Mkutano wa kawaida wa 42 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakimshuhudia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akisaini kitabu cha wageni katika Ubalozi wa Tanzania, DRC.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika kikao kazi na baadhi ya ujumbe wa Tanzania unaoshiriki katika Mkutano wa kawaida wa 42 wa Wakuu wa Nchi na Serikali unaotarajiwa kufanyika Agosti 17 na 18,2022 Jijini Kinshasa, DRC.

Post a Comment

0 Comments