KMC FC watua Arusha kuikabili Coast Union, Polisi Tanzania Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara

NA DIRAMAKINI

KIKOSI cha Timu ya KMC FC ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam chenye wachezaji 24 kimewasili salama jijini Arusha kwa ajili ya michezo miwili ya Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania Bara itakayopigwa Agosti 17 na 21 katika uwanja wa Sheih Amri Abeid jijini humo.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 15, 2022 na Afisa Habari na Mawasiliano wa KMC, Bi.Christina Mwagala.

KMC itakuwa jijini hapo ambapo siku ya Jumatano ya Agosti 17 itashuka katika dimba hilo dhidi ya Coast Union ya mkoani Tanga na Jumapili ya Agosti 21, mwaka huu utakuwa ni mchezo wa pili dhidi ya Polisi Tanzania ambapo katika michezo hiyo yote miwili itakuwa ugenini.

Awali kwa mujibu wa ratiba ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilipanga michezo hiyo miwili dhidi ya Coast kupigwa katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga huku ule dhidi ya Polisi Tanzania ungepigwa katika uwanja wa Ushirika Moshi, lakini kutokana na taarifa ya kufungiwa kwa viwanja hivyo ikapeleka kupangwa katika uwanja wa Sheih Amri Abedi.

Katika msafara huo KMC imewaacha wachezaji wa tatu ambao ni Blase Bigirimana, Waziri Junior pamoja na Eric Manyama ambapo sababu za kutosafiri na timu kwa wachezaji hao ni ni kutokana na kuwa majeruhi ambayo waliyapata wakati wa mazoezi.

Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni chini ya Kocha Mkuu, Thierry Hitimana imejiandaa kikamilifu katika michezo hiyo miwili ambayo itakuwa na ushindani mkubwa kutokana na kwamba kila Timu imejiandaa ipasavyo hivyo mipango na mikakati kama klabu ni kuhakikisha kuwa inapata matokeo mazuri kwenye michezo hiyo ya mwanzo wa Ligi.

“Tumekuja kutafuta alama sita muhimu kwenye michzo hii miwili, tunafahamu ushindani mkubwa utakavyokuwa kwenye michezo hii, lakini kama timu tunapokwenda kuanza ligi tunahitaji ushindi jambo ambalo linawezekana kwa kuwa michezo yote ipo ndani ya uwezo wetu,”ameeleza.

Kwa upande wa afya amesema, wachezaji wote wako vizuri na kila mmoja anamorali na hari ya kuhakikisha kuwa timu inapata matokeo ambayo mashabiki na Watanzania wote wanataka kufurahi, "tunawaheshimu wapinzani wetu, lakini ushindi kwetu ni kipaumbele cha kwanza,"ameongeza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news