Waziri Bashungwa:Bilioni 55/- zitajenga nyumba za walimu 809 nchini

NA OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe.Innocent Bashungwa amesema Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya elimu nchini kwa kuweka mazingira mazuri ya walimu.
Mheshimiwa Bashungwa akitoa salamu.

Mheshimiwa Bashungwa ameeleza hayo leo wakati akitoa salamu ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyoadhimishwa Kitaifa jijini Mbeya huku mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan.
Mheshimiwa Bashungwa akitoa salamu.

Ameeleza pamoja na Serikali kuendelea kuboresha miundombinu ya kujifunzia na kufundishia, katika mwaka wa fedha 2022/23 Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 55.57 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu 809 zenye uwezo wa kuchukua kaya 1,916.

Pia amesema, nyumba hizo zitasaidia walimu kuongeza uwajibikaji zaidi katika kutekeleza majukumu yao.

Vilevile , ameishukuru Serikali kwa kutoa pikipiki 2,500 kwa Maafisa Ugani ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao.
Washiriki katika hafla hiyo.

Akieleza kuhusu Serikali ilivyotoa ruzuku kwa wakulima ya pembejeo, Waziri Bashungwa amemuhakikishia, Mhe.Rais Samia kushirikiana na Wizara ya Kilimo kwa kuwapatia walengwa waliokusudiwa ili wawe ndio wanufaika.

Aidha, ametoa wito kwa wakuu wa mikoa,wilaya na Sekretariti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanasimamia kwa kuepuka wakulima hewa ili lengo la utoaji ruzuku wa pembejeo uendane kusudio.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news