Waziri Simbachawene ahesabiwa na familia yake nyumbani Kibakwe, atoa wito kwa Watanzania

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amehimiza wananchi kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi kwa ajili ya maendeleo yetu wenyewe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akiwa anatoa taarifa muhimu kwa karani wa Sensa ya Watu na Makazi nyumbani kwake Kibakwe Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.

“Unapohesabiwa unakuwa upo katika mpango wako wa maendeleo, katika sehemu yako unayoishi na Nchi kwa ujumla,”amesema.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene baada ya kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi jimboni kwake Kibakwe katika Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akiwa anatoa taarifa muhimu kwa Makarani wa Sensa ya Watu na Makazi nyumbani kwake Kibakwe Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.

Amefafanua kwamba usipohesabiwa, unakosa lile fungu lako katika miaka 10 ijayo kwa ajili ya mipango ya maendeleo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na makarani wa Sensa ya watu na Makazi.

“Bado tuna siku tano mbele kwa ajili ya kuhesabiwa hakikisha umeacha kumbukumbu za watu walilolala usiku wa kuamkia tarehe 23 Agusti 2022,"alisema Waziri.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na makarani wa Sensa ya watu na Makazi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news