Ajali ya Noah yaua wawili, yajeruhi Ikungi

NA DIRAMAKINI

WATU wawili wamefariki dunia baada ya magari aina ya Noah waliokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso eneo la Utaho Barabara Kuu ya kutoka Dodoma kwenda Singida wilayani Ikungi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida , Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Stellah Mutabihirwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea leo Septemba 18, 2022 majira ya mchana katika eneo hilo.

Amesema watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni wanaume akiwemo Katibu wa Msikiti wa Kati (BAKWATA) mjini hapa aliyefahamika kwa jina la Hamisi Dinya ambaye alikuwa akienda kumpokea Mufti wa Tanzania Sheikh, Abubakar Zuberi Bin Ally ambaye ameanza ziara yake leo ya kikazi ya siku mbili mkoani hapa pamoja na mtoto mmoja ambaye jina lake halijafahamika.

Kamanda amesema majeruhi katika ajali hiyo ni saba na walikimbizwa Hospitali ya Misheni ya Puma kwa ajili ya matibabu ambapo hali ya majeruhi mmoja ni mbaya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news