Rais Samia amteua Prof.Janabi kwenda Muhimbili, Dkt.Kisenge achukua majukumu JKCI

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Septemba 18, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi.Zuhura Yunus.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Prof. Mohamed Yakubi Janabi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili. Prof. Janabi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).Prof. Janabi anachukua nafasi ya Prof. Lawrence Maseru ambaye amestaafu.

Pia Mheshimiwa Rais Samia amemteua Dkt. Peter R. Kisenge kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Dkt. Kisenge anachukua nafasi ya Prof. Janabi. Dkt. Kisenge ni Mkurugenzi wa Tafiti na Mafunzo wa (JKCI). Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi huu umeanza Oktoba 2, 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news