Ajali yaua watano, yajeruhi 54

NA DIRAMAKINI

WATU watano wamefariki huku 54 wakijeruhiwa katika ajali ya basi la abiria kugongana na Fuso uso kwa uso eneo la Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga.
Ajali hiyo imetokea leo Septemba 3,2022 majira ya Saa 8 usiku, ikihusisha basi la Kampuni ya Super Najimunisa lenye namba za usajili T.413 DAY likitokea Dar es Salaam kuelekea jijini Mwanza, na Fuso yenye namba za usajili T.123 DJH likitokea Mwanza kwenda Dar es Salaam likiwa na mzigo wa dagaa.

Manusura wa ajali hiyo Fred Mahina, amesema dereva wa basi hilo alikuwa akiendesha mwendokasi na walipokuwa wakimzuia aliwajibu wangetaka usafiri wa raha wangepanda ndege, huku akiwaambia wasali sana ili wafike salama.

"Tulipofika Morogoro dereva akiwa mwendokasi alikwaruza Roli tukapona kuanguka, lakini akazidi kuendesha mwendokasi abiria tulipokuwa tukipiga kelele apunguze mwendo, aligoma na kutuambia tusali ,ndipo tulipofika hapa Shinyanga na kupata ajali," anasema Mahina.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, Leonard Nyandahu ambaye alikuwa eneo la ajali hiyo, amesema chanzo ni uzembe wa dereva wa basi kwa kutozingatia vibao vya usalama barabarani na kuendesha mwendokasi.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga, Dkt. Luzila John amethibitisha kupokea vifo vya watu watano pamoja na majeruhi 54 ambao wanaendelea na matibabu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news