Mzee wa Upako afunguka mazito kuhusu tozo, asema zilianza tangu Torati

NA DIRAMAKINI

ASKOFU wa Kanisa la Gospel Revival Center la Ubungo Kibangu,Anthony Lusekelo, Mzee wa Upako (Chifu Mwantembe) amewataka watanzania kuendelea kuiunga Serikali mkono katika ulipaji wa kodi (tozo) uliotukuka ili kuweza kujenga taifa lenye uchumi imara.
Akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari leo Septemba 3, 2022 ofisini kwake Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam,Mzee wa Upako amesema suala la kulipa tozo lipo toka zamani na hata katika vitabu vya dini limezungumzwa.
“Watu wengi watakuwa wanajua maana ya Zaka na Zabihu, zilichukuliwa kwa wananchi ili kuendesha nchi yao, hivyo mambo ya kuchukua tozo yalianza kutoka mambo ya Torati, hamuwezi kuendesha nchi yenu bila kuchukua nguvu za wananchi wenyewe kwa kuendesha taifa lenu na mambo ya ibada,” amesema Mzee wa Upako.
Mzee wa Upako ameeleza kuwa, katika vitabu vya dini ulipaji wa kodi ulianza mnamo kipindi cha Waisraeli walipokuwa wakihitaji mfalme wao Sauli na kuambiwa wataendesha nchi yao kwa kutozwa kodi ili kuimarisha taifa lao.
Mzee wa Upako alihitimisha mazungumzo yake na wanahabari kwa kusema, "Kulipa kodi ni wajibu wa kila mwananchi katika kujenga Taifa, viongozi wetu wana nia ya dhati kabisa katika taifa hili, hivyo ni wajibu wetu sote kulipa Tozo na Kodi ili kujiletea maendeleo,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news