Balozi Macocha Tembele awasilisha hati za utambulisho kwa Rais Joko Widodo

NA MWANDISHI WETU

BALOZI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Indonesia, Mhe. Macocha Tembele mapema leo Septemba 13,2022 amewasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais wa Indonesia, Mhe. Joko Widodo katika hafla iliyofanyika kwenye Kasri la Merdeka jijini Jakarta.
Balozi wa Tanzania nchini Indonesia Mhe. Macocha Tembele akiwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais wa Nchi hiyo Mhe. Joko Widodo.

Katika hafla hiyo, wawili hao walipata fursa ya kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya biashara na uwekezaji.
Balozi wa Tanzania nchini Indonesia Mhe. Macocha Tembele akiwasili katika Kasri la Merdeka jijini Jakarta ambapo aliwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais wa Indonesia Mhe. Joko Widodo

Hatua hiyo ya Mhe. Balozi Makocha Tembele kuwasilisha hati zake za utambulisho inaashiria kuanza rasmi kwa utumishi wake katika nchi hiyo.
Balozi wa Tanzania nchini Indonesia Mhe. Macocha Tembele akisalimiana na Rais wa Nchi hiyo Mhe. Joko Widodo.

Post a Comment

0 Comments