BREAKING NEWS:Rais Samia atangaza siku tano za maombolezo ya kitaifa

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametangaza siku tano za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha Hayati Malkia wa Uingereza, Elizabeth II, kilichotokea tarehe 8 Septemba, 2022 nchini Uskochi. 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi.Zuhura Yunus, maombolezo hayo yataanza leo Septemba 10, 2022 hadi tarehe 14 Septemba, 2022.

"Katika kipindi chote cha maombolezo, bendera zote zitapepea nusu mlingoti nchini Tanzania zikiwemo kwenye balozi zetu pia.

"Rais Samia amewaomba Watanzania wote kuungana na wenzetu wa Uingereza katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na aliyekuwa kiongozi wao nchini humo,"imeeleza taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news