Dkt.Abbasi:Tanzania Mwenyeji Mkutano wa Music In Africa

NA DIRAMAKINI

KATIBU Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Hassan Abbasi leo Septemba 15, 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Taasisi ya Music in Africa ambao kwa kushirikiana na Wizara pamoja na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wanaandaa Mkutano mkubwa wa sekta ya muzizi Afrika (Music in Africa Conference).

Kikao hicho kimefanyika katika ofisi za Bodi ya Filamu zilizopo Barabara ya Kivukoni, Utumishi jijini Dar es salaam, ambapo Dkt. Abbasi amesema, Tanzania imeteuliwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo utakaofanyika Novemba 24-26, 2022.

"Mkutano huo unatarajiwa kuleta fursa mbalimbali za kukutana na wadau mbalimbali wa muziki kutoka Afrika na duniani kwa ujumla ambapo wasanii mbalimbali watapata nafasi ya kutumbuiza," amesema Dkt.Abbasi.

Amewataka Wasanii na wadau wa muziki nchini kuthibitisha ushiriki wao kupitia mtandao wa @musicinafricaofficial

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news