Makamu wa Rais Dkt.Mpango atoa maagizo kwa Waziri wa Afya

NA DIRAMAKINI

MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Philip Mpango amezindua jengo la huduma za saratani katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando (BMC) jijini Mwanza.

Akizungumza mara baada ya kukagua na kuzindua jengo hilo, Dkt. Mpango amesema, hapa nchini takwimu zinaonesha watu 42,000 hupata ugonjwa wa Saratani kila mwaka kutokana na idadi hiyo Serikali imeamua kuongeza mapambano dhidi ya ugonjwa huo na mengine yasiyoambukiza.

“Serikali imewekeza katika kutengeneza afua mbalimbali za kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza,na miongoni mwa mikakati iliyopo ni pamoja na kupunguza vihatarishi vya magonjwa haya kwa kuelimisha jamii kuchukua hatua stahki za kuboresha mtindo wa maisha kwa kuzingatia ulaji unaofaa, kupunguza matumizi ya pombe, kuacha matumizi ya tumbaku na kufanya mazoezi,”amesema Dkt.Mpango
Dkt.Mpango amesema, pamoja na kukamilika kwa jengo kuna baadhi ya huduma hazitaweza kutolewa kwa sasa kutokana na upungufu wa mashine za mionzi.

“Natoa maelekezo kwa Waziri wa Afya kwa mwaka huu wa fedha kupitia fedha za Global Fund kutoa bilioni 3.1 kwa ajili ya ununuzi wa mashine moja ya mionzi,”amesema Dkt.Mpango.

Dkt. Mpango ameeleza kuwa moja ya mambo yanayosemwa kusababisha saratani katika Ukanda wa Ziwa ni pamoja na kutumia maji machafu kuhifadhi samaki, hivyo ameviomba vyombo vya udhibiti kudhibiti jambo hilo huku akiwaomba wananchi kuacha tabia hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando, Dkt. Fabiani Massaga, amesema ujenzi wa mradi huo ulianza Septemba 1,2020 na umegharimu shilingi bilioni 5.6

Amesema kati ya fedha hizo shilingi bilioni 1.9 zilitoka Serikali Kuu kupitia Wizara ya Afya,bilioni 3.1 ni mchango wa hospitali kupitia mapato ya ndani, wafanyakazi wa hospitali pia walichangia shilingi milioni 250 pamoja na wadau mbalimbali walichangia shilingi milioni 400.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news