Rais Dkt.Mwinyi ateua viongozi mbalimbali leo

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali katika Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Septemba 13, 2022 na Kaimu Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Bw.Masoud H.Iddi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Makame Kitwana Makame kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti.

Makame, kabla ya uteuzi huo alikuwa Mratibu wa Mradi wa IFAD katika Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi.

Pili,Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Said Juma Ali kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Misitu. Kabla ya uteuzi huo, Said alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu.

Tatu, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Dkt.Talib Saleh Suleiman kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (ZALIRI). Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kabla ya uteuzi huo, Dkt.Talib alikuwa daktari na Afisa Mkuu wa Mifugo.

Nne, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Dkt.Mohamed Dhamir Kombo kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (ZARI). Kabla ya uteuzi huo, Dkt.Mohamed alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Mbogamboga na Matunda.

Tano, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua, Mkubwa Ibrahim Khamis kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Zana Nyinginezo za Kilimo. Kabla ya uteuzi huo, Mkubwa alikuwa ni mstaafu katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.

Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi wa Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi kwa viongozi hao unaanza leo Septemba 13, 2022.

Post a Comment

0 Comments