'Mbeya, Iringa, Katavi na Rukwa ukiwekeza fedha zako, unapata faida mara dufu'

NA DIRAMAKINI

LEO Septemba 10, 2022 Watcha Tanzania imeratibu mjadala wa Kitaifa ulioangazia maendeleo na fursa za kiuchumi katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania.

Kupitia mjadala huo ambao umefanyika kuanzia majira ya saa tano asubuhi umejumuisha mikoa ya Iringa, Mbeya, Rukwa na Katavi ambapo viongozi wa mikoa hiyo wameeleza mammbo mbalimbali zikiwemo fursa za kiuchumi kwa ajili ya Watanzania na hata wawekezaji kutoka nje.

MHE.HALIMA OMARI DENDEGO MKUU WA MKOA WA IRINGA

"Kuhusu suala la upatikanaji wa maji katika mkoa wa Iringa zaidi ya asilimia 82.6 maji yanapatikana mijini na asilimia 74.6 maji yanapatikana vijijini na Desemba mwaka huu tunakamilisha miradi ya maji zaidi ya 28.
"Kuhusu suala la nisharti Iringa tupo vizuri kwani tuna vijiji 360 na ambavyo havina umeme ni vijiji 33 tu, hivyo ifikapo mwisho wa mwaka huu umeme kwenye mkoa wetu wa Iringa utakuwa unapatikana kwa asilimia 100.
"Niwaombe wawekezaji kufika Mkoa wa Iringa, kwani una fursa nyingi sana na hata suala la usafiri Mkoa wa Iringa una mtandao wa barabara karibu mikoa yote mikubwa kama Mbeya na Dar es Salaam na pia Serikali inafanya ukarabati Uwanja wa Ndege wa mkoa,"amesema Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Omari Dendego.

MHE.JUMA ZUBERI HOMERA, MKUU WA MKOA WA MBEYA

"Kutokana na juhudi za Mhe.Rais Samia (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan) katika uwekezaji katika sekta ya elimu na hasa ujenzi wa madarasa ya shule za msingi, Mkoa wa Mbeya sasa tunaanza kuona matunda, kwani mkoa wetu umeongeza ufaulu kutoka nafasi ya 13 hadi ya 3 kitaifa katika elimu ya msingi.
"Pia katika elimu ya sekondari zaidi ya shule saba kwenye nafasi za kumi bora zimetoka Mkoa wa Mbeya hili ni jambo kubwa sana kwetu na tunamwahidi Mhe.Rais hatutorudi nyuma kamwe.
"Zaidi ya lita milioni 58 za maji sasa zinapatikana katika Mkoa wa Mbeya ambazo zinanufaisha watu zaidi ya milioni mbili, pia sasa hivi kuna ujenzi wa chanzo kingine cha maji kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Mazingira kitakachokuwa kinatoa lita milioni 1.3,"amesema RC Homera.

MHE. MWANAMVUA MRINDOKO, MKUU WA MKOA WA KATAVI

"Mkoa wa Katavi una umri wa miaka 10 sasa, maana ulianzishwa mwaka 2012 na una jumla ya idadi ya watu ni laki 842,000 kutokana na Sensa ya mwaka 2012, hivyo sensa hii ya 2022 tunategemea ongezeko la idadi ya watu kutokana na watu wengi kutoka mikoa mbalimbali kuvutiwa na shughuli mbalimbali za kiuchumi na jamii.

"Kupitia tozo mbalimbali zinazokusanywa nchini tumeweza kupatiwa fedha hizo kwa jili ya ujenzi wa madarasa zaidi ya 12.
"Kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji tunataarifa kwamba zaidi ya shillingi bilioni tano zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Skimu za Umwagiliaji Mpwampulu iliyopo Manispaa ya Mpanda, hii itasaidia sana ongezeko la mazao mkoani hapa,"amesema RC Mwanamvua Mrindoko.


MHE. QUEEN SENDIGA, MKUU WA MKOA WA RUKWA

"Mkoa wa Rukwa ulianzishwa mwaka 1974 ukimegwa kipande kutoka Mkoa wa Mbeya na Tabora na una jumla ya kilomita za mraba 27.76 huku asilimia 82 ni nchi kavu na asilimia 18 ni maji na hasa kutoka Ziwa Tanganyika na mto Rukwa.

"Serikali imetutengea shillingi bilioni 12.3 kwa ajili ya kuongeza mtandao wa barabara za TARURA huku shilingi bilioni 5 kutoka kwenye fedha hizo ni makusanyo ya Tozo.
"Tumepokea fedha za tozo katika sekta ya afya takribani shilingi bilioni 2.5 ambazo zinaendeleza ujenzi wa vituo vitano vya afya katika mkoa, na vituo hivi vipo katika hatua za mwisho kukamilika,"amesema RC Sendiga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news