Mchechu:Mambo mazuri yanakuja NHC,mtashirikishwa kwa ustawi bora wa makazi Tanzania

NA GODFREY NNKO

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemiah Mchechu amewaeleza wadau wa Sekta ya Milki nchini kuwa, wanakwenda kufanya mapitio ya sera zao ili ziweze kuwapa uwanda mpana wa kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta binafsi katika kuendeleza miradi ya makazi bora nchini.

Ameyasema hayo Septemba 2, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akiwasilisha mipango waliyonayo kwa wadau wa Sekta ya Milki nchini kupitia mkutano wa siku mbili ulioandaliwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambao ulianza Septemba Mosi hadi 2 na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta hiyo nchini.

"Hoja ya pili NHC haiwezi kutatua tatizo hili peke yake, actually nchi hii hata ungekuwa na NHC nyingi ambazo ni efficient hauwezi kutatua tatizo la nyumba kwa Watanzania.

"Lakini tumekuwa tukipata challenge Mheshimiwa Rais (Samia Suluhu Hassan) amezungumza na kutoa maagizo kuona Serikali na taasisi zake zinaingia makubaliano ya public-private partnerships (PPPs), sisi NHC tunaona ni kama fursa kwetu ni nafasi ya kutanua mbawa zetu.

"Kwa hiyo, tunaenda kufanya review ya policy mbalimbali tulizonazo na tulianza joint venture ya mwaka 1993, revise ya 1995, ya 2006 na revise ya 2012 na tunaifanyia revise tena sasa hivi, tunaenda kutengeneza product kama nne ambapo kutakuwa na kongamano rasmi na viongozi wetu. Tutaita wawekezaji ambao wako interested kuwekeza na NHC,"amefafanua.

NHC wana nini?

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemiah Mchechu amesema,"Katika product tulizonazo ya kwanza ni Land as Equity Contribution (LEC) sisi NHC mchango wetu ni ardhi pekee, lakini zao hili tumetengeneza mazao mawili, wale watu wanatamani wawe na milki kubwa mwisho na wale wanaotamani kutengeneza faida.

"Anayetengeneza faida atakuwa na ubia na sisi NHC kwa miaka 25 na baada ya miaka 25 sisi NHC tutabaki na asilimia 75 yeye 25 tunapoanza tunaanza na asilimia 25 to 75 na hii inakuja kwenye faida tunayotengeneza.

"Sisi tunachukua apartments zetu kadhaa na yeye tunamwachia asilimia 75 baada ya miaka 10 NHC tunaongeza asilimia 25 yeye anapunguza 25 percent tunakuwa tuko 50 kwa 50, baada ya miaka 10 tena tunachukua another asilimia 25 yeye asilimia 75 maana yake two at three end ya miaka 25 sisi tunachukua asilimia 75 yeye anabaki na asilimia 25 lakini kikubwa atakuwa anapata faida ya kutosha kabla hajafikia mahali hapo.

"Sasa tumepiga mahesabu hadi tunapokuja na hizi numbers na tumeangalia experience ya nyumba zetu tunapokuwa tunazicharge ni kutegemeana na maeneo na maeneo.

"Maeneo yenye high ritani actually unarahisisha wawekezaji wako 100 percent kwenye mwaka wa 9-11 hasa Kariakoo na Kariakoo unatengeneza hela yako ya pili, yale maduka ni vidogo lakini angalia kodi zinazochangiwa convert katika dola, Kariakoo square mita moja ni dola 60, lakini pana faida na watu wananunua kwa ajili ya biashara au kupanga kwa ajili ya biashara hii inamgusa mtu ambaye amekuja kwa ajili ya biashara na kuwekeza," amefafanua Bw.Mchechu.

Bw.Mchechu anaendelea kufafanua kuwa, "Lakini kuna mwingine yeye na hela yake lengo lake ni kwamba angetamani walau kizazi chake kiwe na eneo walau eneo la Kariakoo au katikati ya mji wowote maeneo ya Tanzania, kwa sababu hii sera inakwenda kutumika kila sehemu ya ndani ya nchi ya Tanzania iwe ni Musoma, Ruvuma au Mtwara.

"Hii ya pili kwa mtu anayetamani abaki na reasonable stake huyu hata enjoy mpaka miaka 25, huyu ataenjoy miaka 15 na baada ya miaka 15 NHC tunakuwa na 50 percent yeye 40 percent life time, sasa hizi sera siyo Static na sisi tutakuwa tunaenda tunabadilisha depending na responses ya business slient na feedback tunazozipata kwa hiyo katika hii sera ya mwisho mtu ataanza na 25 percent to 75 percent baada ya miaka 10 vile vile NHC watapata 25 percent kwa hiyo itakuwa ni 50 to 50 percent.

"Na baada ya miaka mitano zaidi tuna earn ten more shares ambayo itakuwa ni 60 yeye ana 40 na hii inakuwa ni life time, lakini kikubwa hapa tuna dis-engage katika mwaka wa 15, lakini huku ulikuwa una enjoy mpaka mwaka wa 25 ndio maana nasema hii moja imeangalia biashara foward to the end shares holding yako inakuwa ndogo, hii nyingine imeangalia land ownership, kwa sababu ni muda mfupi, lakini unakuwa na reasonable large shares ya 40 percent na kuna vigezo ambavyo vipo katika zoezi hilo.

"Ya pili tunaita ni Land and Finance as Equity Contribution kwa maana ya kwamba NHC tuna uwezo wa kuchangia ardhi na pesa, lakini katika hili tunajikita katika miradi mikubwa. Hatutaki kujumuisha kila mradi wa private sector. Mfano una mradi wako mdogo wa bilioni 5, 10, au 30 kwamba unaweza ukafanya, tunasema hapana, mradi wa shilingi bilioni 50 sisi tunaweza tukaingia tukachangia ardhi, fedha na mwekezaji analeta fedha.

"Katika hili tunafuata vigezo vyetu vikubwa, lazima tujihakikishie internal rate of ritani of minimum ni 12 percents na pia pay back period ya mradi wote is not more than 12 years, tunaweka sehemu ambayo tuna uhakika kuna efficient ndipo tunaweka pesa yetu, tuna wajibu wa kuhakikisha tunachambua, kukagua na kuhakikisha interest ya Serikali na wananchi wake inatunzwa katika maamuzi tunayoyafanya.

"Ya tatu inaitwa revenue sharing model, hii ni ile mwekezaji anakuja anataka ashirikiane na NHC lengo lake ajenge na kuuza ule mradi 100 percents, kama sisi tunavyojenga affordable apartments lengo letu kuzijenga na kuziuza. Kumbe ukiona tumepangisha tumekosa wateja, lakini lengo ni kujenga na kuuza.

"Katika hili mojawapo ya kigezo kikubwa sana tunachoangalia ni project ambayo NHC unai-commit minimum lazima iwe mara mbili ya thamani ya ardhi, wewe tuletee ile business plan yako, walau inaonesha utakachotugawia sisi kwa faida kina thamani mara mbili ya ardhi ile kibiashara inakuwa imefanyika soko la ardhi tunasema mfano hii ardhi ni shilingi bilioni mbili, maana yake nikienda sokoni ni shilingi bilioni mbili hiyo ndio nitapata, lakini wewe kwa kuongeza jengo ukatengeneza faida na sisi ukatugawia shilingi Bilioni mbili zaidi tukawa na shilingi bilioni nne, we can go.

"Lakini ili tuwe na uhakika zaidi na decision tuliyofanya ni sawa, tunahakikisha kwenye RCM (Reliability Centered Maintenance) unatuletea proposal yako, tunajaribu kuweka open kuangalia watu wengine nani anaweza akatupa faida kubwa ndiye tutakwenda naye na ikionekana hayupo yaani hakuna mwingine basi tunakwenda na wewe, lakini kigezo kikubwa the minimum must be twice.

"Nyingine ni long term Lease Agreement, ni pale ambapo unataka ufanye mwendelezo fulani na katika huo mwendelezo baada ya muda, yale mwendelezo yanakuwa mali ya NHC 100 percent na tutakubaliana unatulipa kodi fulani na katika hii tunasema kwamba itakuwa inaingiwa na mkataba kati ya miaka 10 hadi 30 kutegemeana na size na nature ya mwekezaji.

"Hiki ndicho kinaenda kufanyika, zote hizi kuna vigezo sasa ambavyo vinafanyika kufahamu mteja ni nani kama ardhi yetu ni shilingi bilioni mbili wekeza zaidi ya shilingi bilioni mbili walau bilioni nne, sio ardhi yetu bilioni mbili unajenga mradi wa bilioni 1.5 NHC itakuwa inaingia hasara, tutaangalia share contribution revenue na shares risk,"amesema Mchechu.

Mkurugenzi Mkuu huyo wa NHC amesema kwamba, uzinduzi wa mpango huo utafanyika hivi karibuni jijini Dar es laam, Arusha na Mwanza kwani rasilimali nyingi za shirika hilo ziko katika mikoa hiyo.

Pia amesema,ushiriki wa sekta binafsi kwa kushirikiana na NHC utasaidia kutekeleza ujenzi wa miradi mingi ya makazi itakayoleta hadhi katika miji mbalimbali na kuchochea uchumi na maendeleo.

Aidha ameongeza kuwa, NHC imedhamiria kuleta mapinduzi chanya katika ujenzi wa makazi ambayo yatakuwa nafuu na himilivu kwa kuwa na bei isiyozidi shilingi milioni 200 sambamba na kuendeleza maeneo ya NHC hapa nchini.

Miradi mingine

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemiah Mchechu ameendelea kufafanua kuwa, miradi ambayo wanakwenda nayo ni pamoja na mradi wa Safari City jijini Arusha na kwamba Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa sasa wanatengeneza daraja nyuma ya Uwanja wa Ndege wa Arusha kwenda katika viwanja hivyo ambavyo vimepimwa.

Pia amesema, Mradi wa Salama Creek uliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam ambapo NHC wana hekta zaidi ya 200 master plan tayari imeshafanyika japo hawajauweka katika bajeti ya mwaka huu wa fedha na kwamba wanakusudia kuangalia namna ambavyo watashirikiana na wawejezaji wakawekeze, lengo nyumba zijengwe.

Aidha, mradi mwingine ni mradi wa Seven Eleven Kawe (NHC Plot 711-Kawe Beach) ambao ulikwama kidogo katika ghorofa ya 12.

"Kwa sasa tupo hatua ya mwisho kujenga jumla ya apartments 420 na ndani ya muda mchache mkandarasi atapewa mkataba, utakuwa na makazi, maduka na juu kuna viwanja vya michezo na itachukua jumla ya idadi ya watu 420,"amesema.

Mchechu akizungumzia upande wa Mradi wa Morocco Square amesema, mwezi Novemba utakuwa tayari na una wapangaji asilimia 65 na kwamba kazi za ndani zinafanyika, "kwa sasa apartments bado zipo za middle na high classes na kuna kumbi nne za sinema kila kumbi itachukua watu 100 hadi 181,"amesema.

Wakati huo huo,Mchechu amesema kwa upande wa mradi wa Magomeni, Kinondoni kwa Manyanya anaomba sekta binafsi kushiriki katika ujenzi wa makazi na miradi na kwamba NHC itakuwa na kitengo maalumu kitakachokuwa kikiwaeleza watu juu ya mikopo na kutoa mwongozo kati ya wateja wao na benki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news