Mnadhimu Mkuu wa JWTZ afanya ziara maalumu CAR

NA DIRAMAKINI 

MNADHIMU Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Luteni Jenerali Salum Haji Othman amefanya ziara maalum katika Kikosi cha Walinda Amani kutoka Tanzania kinachohudumu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Luteni Jenerali Salum Othman akiwa na ujumbe wake wamewasili katika Uwanja wa Ndege wa Berberati uliopo katika mkoa wa Mambere Kadei na kupokelewa na mwenyeji wake Kamanda Kikosi TANBAT 05 Luteni Kanali Adam Hamis Kiza, maafisa na askari mbalimbali wanaohudumu katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa (MINUSCA) katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Luteni Jenerali Othman amepokelewa na gwaride la heshima lililoandaliwa na TANZBAT 5 na baadae kupokea taarifa ya utendaji kazi ya Kikosi kutoka kwa Afisa Mkuu wa Operesheni Meja Amulike Kabale.

Pamoja na mambo mengine Luteni Jenerali Salum Othman amepata wasaa wa kufanya mazungumzo na Kamanda Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi wa Amani (MINUSCA) Luteni Jenerali Sidiki Traole yanayolenga utendaji kazi wa Kikundi cha walinda amani wa Tanzania.

Pia amepata fursa ya kufanya mazungumzo na maafisa na askari katika ukumbi wa Serengeti ambapo walinda amani hao walionesha ari, hamasa na utayari wa kutekeleza majukumu ya ulinzi wa amani huku wakifuata sheria na taratibu za Umoja wa Mataifa, pamoja na za nchi husika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news