Prof.Muhongo akagua sehemu ya ujenzi wa barabara ya kwanza ya lami jimboni

NA FRESHA KINASA

MRADI wa ujenzi wa barabara ya lami ya Musoma-Makojo-Busekera kilomita 92 unaanza kuweka matumaini makubwa kwa wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini Mkoani Mara.

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo mwenye kofia wakikagua barabara.

Ambapo kilomita tano zitakamilika ifikapo Oktoba 30, 2022 baada ya Kampuni ya Gemen Engineering inayojenga kilometa hizo tano chini ya Mkurugenzi wake Mhandisi, Andrew Nyantori kubainisha hayo.

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mheshimiwa Prof. Sospeter Muhongo, Septemba 14, 2022 alikagua ujenzi wa barabara hiyo ili kujiridhisha na ahadi ya Mkandarasi huyo.

Barabara hiyo inatajwa kuwa na umuhimu mkubwa kwani ndiyo roho ya ukuaji wa uchumi wa Jimbo la Musoma Vijijini lenye kata 21, Vijiji 68 na Vitongoji 374. Kwani samaki wengi na wa aina mbalimbali wanaovuliwa Ziwa Victoria wanasafirishwa kutoka Musoma Vijijini kwenda kwenye masoko mbalimbali ya ndani na ya nje ya nchi kwa kutumia barabara hiyo.

Aidha, mazao ya chakula ambayo nayo ni ya biashara kama mihogo, mahindi, viazi vitamu, mpunga na matunda yanasafirishwa kutumia barabara hiyo ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa maendeleo ya uchumi wa wananchi wa Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara na Tanzania kwa ujumla.

"Musoma Vijijini ni maarufu kwa kilimo cha pamba, barabara hili ndiyo inatumika kusafirisha pamba kutoka vijijini mwetu kwenda sokoni. Dhahabu na madini mengine yanayochimbwa Musoma Vijijini yanasafirishwa kwa kutumia barabara hili.

"Umuhimu wa barabara hili kwa huduma za kijamii. Hili ndilo barabara kuu na pekee linalounganisha vijiji vyote 68 vya jimboni mwetu. Kwa hiyo, hii barabara ni muhimu sana kwa usafiri wa wananchi ndani na nje ya jimbo letu. Na pia ndiyo barabara kuu na pekee ambayo inatumika kwa usambazaji wa vifaa vya elimu, huduma za afya, kilimo, ufugaji, maji, umeme, ndani ya jimbo letu.

"Wagonjwa wanaohitaji matibabu kwenye hospitali kubwa za Musoma, Mwanza na nyinginezo wanatumia barabara hii.

"Ombi kwa serikali, kasi ya ujenzi iongezeke kwa kuongezewa bajeti ya utekelezaji wa ujenzi wa barabara hili," imeeleza taarifa ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

Japhet Majura ni Mkazi wa Musoma Vijijini ambapo ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuijenga barabara hiyo, kwani itakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi katika kuchochea maendeleo yao kwa shughuli za kiuchumi na kijamii.

Naye Felista Magesa ameshukuru mpango wa serikali wa kuijenga kwa lami barabara hiyo, kwani ni jambo la kupongeza na kwamba itazidi kukuza uchumi wa wananchi jimboni humo.

Vedastus Malibe ni Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mara ambapo amemhakikishia Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof.Muhongo kuwa, barabara hiyo itajengwa kwa ubora unaotakiwa na kwamba makao makuu ya Halamashauri hiyo wataweka barabara za lami.

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Mheshimiwa Prof.Sospeter Muhongo amesema kuwa, kwa Jimbo la Musoma Vijijini hiyo ndiyo lami ya kwanza, hivyo wananchi wana furaha kuona ujenzi huo ukiendelea vizuri.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news