Prof.Muhongo awasilisha tena maombi ya usambazaji umeme vitongoji ambavyo bado jimboni

NA FRESHA KINASA

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, Mheshimiwa Prof.Sospeter Muhongo amefanya kikao na viongozi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) makao makuu Dodoma na kuwasilisha tena maombi ya usambazaji wa umeme kwenye vitongoji ambavyo bado havijaunganishiwa umeme ndani ya jimbo hilo.

Hayo yamebainishwa leo Septemba 22 , 2022 kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini ikielezea hatua hiyo muhimu iliyofanywa na mbunge huyo Mheshimiwa Prof. Sospeter Muhongo.
Ambapo taarifa hiyo imesema kuwa, REA imepokea maombi hayo na itaendelea na usambazaji wa umeme kwenye vitongoji ambavyo bado havijaunganishiwa baada ya kukamilisha taratibu za upatikanaji wa fedha za Miradi ya Umeme Vijijini.

Aidha, tayari wataalam wa REA wameshatembelea vijiji vyote 68 na kuanisha vitongoji ambavyo bado havijaunganishiwa umeme. Na kazi hiyo waliifanya kwa kushirikiana na madiwani na wenyeviti wa Serikali za vijiji ili vitongoji vingi ambavyo bado jimboni humo viweze kuunganishiwa umeme.

"Ifahamike kuwa, miundombinu ya umeme jimboni mwetu vijiji vyote ni 68 vimeunganishwa kwenye gridi ya umeme ya taifa, yaani miundombinu ya usambazaji wa umeme ipo kila kijiji na ukubwa wa jimbo letu kata 21, vijiji 68 na vitongoji 374," imeeleza taarifa hiyo.

Post a Comment

0 Comments