Rais Dkt.Mwinyi ashiriki kuchagua viongozi wa chama Jimbo la Mpendae, atoa wito

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Mwinyi leo ameshiriki katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ngazi ya jimbo uliofanyika ofisi za Jimbo la Mpendae Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akipiga kura kumchagua Mwenyekiti na Viongozi wa CCM Jimbo la Mpendae Unguja, uchaguzi umefanyika leo katika ukumbi wa Tawi la CCM Mpendae.(Picha na Ikulu).

Akitoa nasaha kwa wajumbe wa mkutano huo, Dkt.Mwinyi aliwataka kutumia vyema demokrasi kwa kuchagua viongozi kwa busara kubwa na kuzingatia wanachama wenye uwezo, uadilifu na wanaokataa rushwa.
Katika mkutano huo wajumbe walipata fursa ya kupiga kura na kuchagua viongozi mbalimbali katika nafasi ya Mwenyekiti wa Jimbo, Katibu wa Jimbo pamoja na Katibu wa Siasa na Uenezi wa jimbo hilo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Mpendae Unguja, baada ya kupiga kura kuwachagua viongozi wa CCM Jimbo la Mpendae uchaguzi uliyofanyika leo katika ukumbi wa Tawi la CCM Mpendae.

Nafasi nyingine zilizogombewa ni pamoja na wajumbe watatu watatu wa Mkutano Mkuu wa Mkoa, wajumbe watano wa Halmashauri Kuu ya Wilaya pamoja na wajumbe watano wa Halmashauri Kuu ya jimbo.

Post a Comment

0 Comments