Rais Samia awaagiza Wakuu wa Mikoa kusimamia lishe bora

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaagiza Wakuu wa Mikoa kuhakikisha fedha zilizopangwa kutekeleza mipango ya lishe zinatolewa kwa wakati.
Rais Samia ametoa agizo hilo leo wakati akihutubia Mkutano wa Mwaka wa Tathmini ya Sita ya Mkataba wa Lishe uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji, Mtumba.

Aidha, Rais Samia amesema kuwa mpango wa lishe mikoani hautekelezwi ipasavyo hivyo Wakuu wa Mikoa wanapaswa kujipanga na kuongeza jitihada za kuhamasisha utekelezaji wa shughuli za lishe bora na kuzipa kipaumbele ili zilete tija.
Makatibu Tawala pamoja na viongozi wengine wakiwa kwenye hafla ya uwekaji wa saini Mikataba ya Usimamiaji wa Shughuli za Lishe iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Kutokana na hilo, Rais Samia amemuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, kuwachukulia hatua stahiki Viongozi ambao wamefanya ubadhirifu wa fedha za lishe.

Rais Samia ameelekeza sekta zinazoguswa na utapiamlo ikiwemo kilimo, mifugo, viwanda, afya na biashara kuweka mikakati ya kuhakikisha vyakula vinavyohitajika katika kukamilisha lishe vinapatikana na kuviongezea virutubisho hasa katika ngazi za chini.
Wakuu wa Mikoa wakiweka saini Mikataba ya Usimamiaji wa Shughuli za Lishe katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Hali kadhalika, Rais Samia ameiagiza Wizara ya Afya kuifanyia mabadiliko Sera ya Taifa ya Lishe ya mwaka 1992 ambayo imepitwa na wakati ili iendane na hali halisi na mipango ya sasa hivi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news