Serikali kupitia eGA yawapatia mafunzo ya TEHAMA vijana wa vyuo vikuu

NA VERONICA MWAFISI

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi, amesema serikali kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) imewapatia mafunzo ya TEHAMA vijana wa vyuo vikuu ili kuwajengea uwezo utakaosaidia kuleta maendeleo ya TEHAMA nchini ikiwa ni pamoja na kuwaandaa vijana hao kutoa mchango katika utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na vijana wa Vyuo Vikuu waliokuwa wakifanya utafiti na ubunifu wa mifumo ya TEHAMA kupitia Kituo cha Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa Mifumo cha Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) wakati akifunga mafunzo kwa vijana hao jijini Dodoma.

Mhe. Ndejembi amesema hayo jijini Dodoma, wakati akifunga mafunzo ya TEHAMA kwa vijana hao wa vyuo vikuu yanayotolewa kupitia Kituo cha Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa Mifumo cha Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA).

Naibu Waziri Ndejembi amesema, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan imeelekeza nguvu nyingi katika utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali ambao unahitaji wataalam na ndio sababu ya serikali kutoa mafunzo ya TEHAMA kwa vijana ya vyuo vikuu.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza wakati akifunga mafunzo kwa vijana wa Vyuo Vikuu waliokuwa wakifanya utafiti na ubunifu wa mifumo ya TEHAMA kupitia Kituo cha Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa Mifumo cha Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) jijini Dodoma.

“Ninyi vijana mliopatiwa mafunzo kupitia kituo hiki cha Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa Mifumo cha eGA ndio wataalam mnaotegemewa kutoa mchango ili kufikia lengo la Mhe. Rais la kuwa na Tanzania ya Kidijitali,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.
Vijana wa Vyuo Vikuu waliokuwa wakifanya utafiti na ubunifu wa mifumo ya TEHAMA kupitia Kituo cha Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa Mifumo cha Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati akifunga mafunzo hayo ya ubunifu na utafiti jijini Dodoma.

Mhe. Ndejembi ameongeza kuwa, uwepo wa kituo hicho cha Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa Mifumo ni sehemu ya utekelezaji wa azma ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwa na kituo kitakachokuwa ni kitovu cha kukuza vipaji katika eneo la TEHAMA.

Mhe. Ndejembi ameipongeza Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) kwa kuanzisha kituo hicho kitakachosaidia kufikia lengo la Mhe. Rais la kuzalisha wataalam wengi wa TEHAMA ambao watakaotoa mchango katika kubuni mifumo imara itakayoboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Mhandisi Benedict Ndomba akiwasilisha taarifa kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi kuhusu utekelezaji wa kazi za utafiti na ubunifu wa mifumo ya TEHAMA zilizokuwa zikifanywa na Vijana wa Vyuo Vikuu kupitia Kituo cha Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa Mifumo cha Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) jijini Dodoma.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Mhandisi Benedict Ndomba amesema, suala la utafiti na ubunifu limepewa kipaumbele na eGA katika kuendeleza jitihada za serikali mtandao ndio maana ilianzisha Kituo cha Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa Mifumo ya TEHAMA ambacho ndani ya muda mfupi kimekuwa na faida katika kukuza vipaji vya vijana wa Vyuo Vikuu kwenye eneo la TEHAMA.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cosmas Ngangaji akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi kuzungumza na Vijana wa Vyuo Vikuu waliokuwa wakifanya utafiti na ubunifu wa mifumo ya TEHAMA kupitia Kituo cha Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa Mifumo cha Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) jijini Dodoma.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Cosmas Ngangaji amesema kuwa, kazi ya utafiti na ubunifu wa mifumo inayofanywa na vijana hao wa vyuo vikuu waliopatiwa mafunzo ya TEHAMA, itasaidia kurahisisha utendaji kazi wa serikali na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Mmoja wa vijana wa Vyuo Vikuu wanaopatiwa mafunzo ya utafiti na ubunifu wa mifumo ya TEHAMA kupitia Kituo cha Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa Mifumo cha Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Bi. Osrida Efraim akishukuru kupata fursa ya kujifunza kwa njia ya vitendo katika Kituo hicho wakati Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi alipokuwa akifunga mafunzo hayo jijini Dodoma.

Mmoja wa vijana wa vyuo vikuu walionufaika na mafunzo yanayotolewa katika Kituo cha Utafiti na Ubunifu wa Mifumo cha eGA, Bi. Osrida Efraim amesema kuwa, amepata ujuzi wa masuala ya TEHAMA ambao utamuwezesha kutoa mchango katika kubuni mifumo ya TEHAMA itakayoboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Mnufaika mwingine wa kituo hicho, Bw. Mpotisambo Zamea amesema ujuzi alioupata utamuwezesha kutoa mchango kwa serikali katika usimamizi wa mifumo ya TEHAMA ya utoaji huduma kwa umma, ikiwa ni pamoja na kuimarisha usalama wa mifumo hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya vijana wa Vyuo Vikuu wanaofanya utafiti na ubunifu wa mifumo ya TEHAMA kupitia Kituo cha Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa Mifumo cha Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) mara baada ya kufunga mafunzo hayo ya utafiti na ubunifu jijini Dodoma. Wa kwanza kushoto kwake ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cosmas Ngangaji na wa kwanza kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) Mhandisi Benedict Ndomba.

Kituo cha Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa Mifumo cha Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) kilichoanzishwa kwa ajili ya kupokea wanafunzi wa mazoezi kwa njia vitendo kutoka katika vyuo vikuu kinaendelea kutoa mafunzo kwa vijana wa vyuo hivyo watakaopata fursa ya kuchaguliwa, ili wawe na ujuzi utakaokuwa na tija katika kubuni mifumo ya TEHAMA itakayowezesha kufikia lengo la serikali la kuwa na mifumo imara itakayoboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news