NA DIRAMAKINI
LEO Septemba 24, 2022 viongozi wa mikoa ya Songwe, Geita na Simiyu wameshiriki mjadala wa Kitaifa juu ya maendeleo na fursa za kiuchumi zinazopatika katika mikoa hiyo.

MHE.YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA WA SIMIYU
"Mkoa wa Simiyu ulipokea fedha nyingi zaidi kwa mwaka fedha 2021/2022 ulipokea karibia shilingi bilioni 29 kwa ajili ya utekelekezaji wa miradi ya maendeleo kwa upande wa barabara tulitengewa shilingi bilioni 14 na zilikuja shilingi bilioni 12, na kilomita 925 na madaraja 43 yalitengenezwa, 2022/ 2023 mkoa ulitengewa zaidi shilingi bilioni 11 kwa ajili ya miradi ya barabara.



MHE.MARTIN REUBEN SHIGELA, MKUU WA MKOA WA GEITA
"Jambo zuri hapa Geita tuna Hospitali Rufaa ya Chato ambayo ni kubwa na kwa sasa imekua kama ya Kimataifa kwa sababu tunapokea wagonjwa kutoka baadhi ya nchi zinazotuzunguka kama Burundi, Rwanda na Uganda na kikubwa wanachokifuata ni huduma zetu bora.



MHE.WAZIRI WAZIRI KINDAMBA, MKUU WA MKOA WA SONGWE
"Songwe tuna usemi usemao ONGWE NI LAKO KUU LA SADC, kwa sababu majirani zetu wa nchi jirani wanatumia Mkoa wa Songwe kama njia ya kupitishia mizigo yao na sababu kubwa wenzetu hawana Bandari.
"Tunawakaribisha Watanzania kuja kuwekeza kwenye Sekta ya Uvuvi, kwa sababu sisi hapa Songwe tunapakana na Ziwa Rukwa ambalo linatoa samaki wazuri na watamu, lakini pia kuna fursa ya ufugaji wa nyuki,"amesema.

"Sekta ya Afya hapa Songwe imepokea zaidi ya shilingi Bilioni 44 ambazo zimegawanywa kwenye maeneo mbaimbali ikiwemo Eneo la Mama na Watoto, Ununuzi wa Vifaa Tiba, Ujenzi wa Hospitali na Vituo vya Afya,"amesema.