Tanzania kuiunganisha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mkongo wa Taifa

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mheshimiwa Nape Nnauye amesema, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajia kuiunganisha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Mkongo wa Taifa ili kuipatia huduma ya intaneti.

Mheshimiwa Waziri Nape ameyasema hayo leo Septemba 26, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo litakalofanyika Oktoba 18 hadi 19, mwaka huu kwa lengo la kukuza matumizi ya TEHAMA.

“Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo itakuwa ni nchi ya nane kuunganishwa na Mkongo wa Taifa kwani kwa sasa tumeshaunganisha kwa nchi saba,”amesema Waziri Nape.

Akizungumzia kongamano hilo, Mheshimiwa Nape amesema moja ya mkakati wa Serikali ya Tanzania ni kuhakikisha inaongeza matumizi ya TEHAMA kwa kuweka mazingira wezeshi ya kisera na kisheria.

Post a Comment

0 Comments