TFF yapitisha usajili wa Twisila Kisinda kuichezea Yanga SC

NA DIRAMAKINI

KAMATI ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepitisha usajili wa Twisila Kisinda kuichezea Yanga baada ya klabu hiyo kumuhamisha mchezaji wake wa kigeni Lazarous Kambole.

Kambole amejiunga na timu ya Wakiso Giants inayocheza Ligi Kuu ya Uganda, na tayari TFF imetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC).
Awali Kamati hiyo ilizuia usajili wa Kisinda licha ya kuwa ulifanyika ndani ya dirisha la usajili kwa vile tayari Yanga ilikuwa na wachezaji 12 wa kigeni.

Licha ya changamoto hiyo, pia Kisinda aliombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ambayo tayari imepatikana.

Hivyo kwa kumuhamisha Kambole imepata nafasi ya kumsajili Kisinda kama ilivyokuwa imeshauriwa huko nyuma. 

Kwa mujibu wa Kanuni ya 62(1) ya Ligi Kuu Toleo la 2022, klabu inaruhusiwa kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi 12.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news