'Uigeuze mioyo ya viongozi wa Serikali na kanisa wawatendee wanyonge kwa huruma'

NA ADELADIUS MAKWEGA

VIONGOZI wa Serikali na Kanisa wameombewa kugeuza mioyo yao na kukumbuka kuwatendea kwa huruma kila yanayoamuliwa dhidi ya maamuzi mbalimbali yanayofanywa kila siku kwa wanyonge.

“Uigeuze mioyo ya viongozi wa serikali na kanisa ili wawatendee wanyonge kwa huruma”. Maombi haya yalifanyika katika misa ya Jumapili ya 24 ya mwaka C katika Kanisa la Bikira Maria Immakula Parokia ya Chamwino Ikulu Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma, Septemba 11, 2022.

Kabla ya maombi hayo misa hiyo iliyoongozwa na Padri Paul Mapalala alipohubiri, alisisitiza juu ya huruma ya Mungu kwa wanadamu huku akisisitiza kukumbuka kuombana misamaha tunapokosea.

“Masomo yote matatu ya Jumapili ya leo, kwa miaka yote yanatoa simulizi ndefu ya muinjili Luka na yanaonesha huruma ya Mungu kwetu sisi wanadamu ambao mara nyingi tu wakosaji na wapotevu, simulizi hii ndefu ya injili inaeleza kati ya baba na watoto wake wawili, aliyekuwa anamtii na yule aliyekwenda mbali kufanya maisha yake ya peke yake, huko yakamshinda na kurudi, fundisho lake ni kuwa Mungu wetu ni mwenye huruma, tukirudi kwake atatusamehe tu.”

Akiendelea kuhubiri katika misa ya kwanza, Padri Mapalala aliongeza kuwa, “Mungu mara zote yupo tayari kutupokea pale tunapomrudia, isipokuwa ni kiburi chetu, uhuni wetu, upumbavu wetu na ujinga wetu, kama ilivyokuwa kwa mtoto wa pili katika injili hii, unapokuwa na kiburi Mwenyezi Mungu hawezi kukupokea kwa sababu yeye ndiye aliyekuumba, yeye ndiye aliyekuleta duniani yeye ndiye atakayekupatia yote, uweze kutekeleza na unapokwenda kinyume, tafakari, fikiri mara nyingi, iwe kwa mwezio wa ndoa, kwa mzazi wako na kwa watu mnaofanya nao kazi pamoja, ombaneni misamaha.”

Misa hiyo ilifanyika katika hali ya baridi kali katika eneo hilo ambayo imedumu kwa muda mrefu kwa nyakati za asubuhi na usiku huku kwa desturi mkoani Dodoma baridi huwa kali sana mwezi wa sita pekee.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news