Waziri Balozi Dkt. Chana ateua wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA)

NA DIRAMAKINI

KUFUATIA Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumteua Meja Jenerali (mstaafu) Hamis R. Semfuko kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi H. Chana (Mb) kwa mamlaka aliyopewa chini ya Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori Namba 5 ya mwaka 2009, Sura 283 ikisomwa pamoja na Kipengele cha 3.1.1 (b) cha Amri ya Uanzishwaji Uhifadhi wa Wanyamapori amewateua wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).

Wajumbe walioteuliwa kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Septemba 19, 2022 na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Maliasili na Utalii ni;

1:Prof. Jafari R. Kideghesho - Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka, Moshi.

2:Dkt. Simon R. Mduma - Mkurugenzi Mkuu (Mstaafu), Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).

3:Prof. Susan Augustino - Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA)

4:Bi. Beatrice Raphael Kimoleta - Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

5:Bw. Simon Thomas Chillery - Naibu Kamishna wa Polisi, Jeshi la Polisi Tanzania.

6. Dkt. Maurus January Msuha - Mkurugenzi wa Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii. Bw. Elirehema Aminiel Nyiti - Afisa Mwandamizi Ofisi ya Rais, Ikulu.

Aidha, Bw. Mabula Misungwi Nyanda, Kaimu Kamishna wa Uhifadhi - TAWA atakuwa Katibu wa Bodi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi huu ni wa miaka mitatu kuanzia leo Septemba 19, 2022 hadi 18 Septemba, 2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news