WAZIRI BALOZI MULAMULA:TUNATHAMINI NA KUTAMBUA MCHANGO WA INDIA

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amesema Tanzania inathamini na kutambua mchango mkubwa wa India katika kuendeleza miradi ya maji na afya nchini.
Balozi Mulamula ametoa kauli hiyo katika hafla ya kuadhimisha miaka 75 ya Jamhuri ya India katika Umoja wa Mataifa iliyofanyika jijini New York kwenye Ofisi za Ubalozi wa kudumu wa India katika Umoja wa Mataifa.

“Tanzania inathamini na kutambua mchango wa India katika kuisaida serikali kutekeleza mipango yake ya maendeleo, na tunaamini kuwa ushirikiano uliopo utakuwa zaidi na zaidi kwani ushirikiano huo ni matunda ya uhusiano wa nchi za kusini na kusini,”
Amesema, uhusiano na Indi unachangia juhudi za Tanzania kufikia malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa ya Afya na ustawi wa watu na maji safi na salama na hivyo kuchangia utekelezaji wa dira ya Tanzania ya mwaka 2025 na kuongeza kuwa ni mmoja ya wawekezaji wakubwa nchini ambaye anachangia asilimia 16 ya biashara ya Tanzania na kuchagiza utekelezaji wa dira yetu ya 2025.
Ametaja miradi inayonufaika na ushirikiano huo kuwa ni usambaza maji Dar es Salaam hadi Chalinze wenye thamani ya Dolla za Marekani Milioni 178 ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka huu. 

Miradi mingine ni usambazaji wa bomba la maji kutoka Ziwa Victoria hadi Tabora, Igunga, na Nzega uliozinduliwa mwezi Januari 2021; kusambaza bomba la maji kwenda katika miji ya Tinde na Shelui na vijiji vya jirani wenye thamani ya dola milioni 10.64 za Marekani ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba 2022.

Pia kuna na mradi wa ujenzi wa mfumo wa usambazaji maji katika miji 28 Tanzanian wenye thamani ya dola milioni 500 za Marekani ambao utekelezaji wake unatarjiwa kuanza mwezi Disemba 2022.
Kuhusu sekta ya Afya Balozi Mulamula amesema Tanzania inaishukuru India kwa mchango wake kwa Tanzania kujiweka tayari kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID 19 hasa kwa kuwekeza katika ujenzi wa vituo vya afya, kuongeza nguvu ya watumishi wa afya nchini na kuongeza uwezo wa nchi kutengenza dawa, ugavi, chanjo na vifaa tiba.
Tarehe 15 Agosti India iliadhimisha miaka 75 ya kuwa Jamhuri na miaka 76 tangu ipate uhuru kuadhimisha miaka 75

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news