Waziri Dkt.Kijaji:Serikali itaendelea kutekeleza Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara nchini (Blueprint)

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe.Dkt.Ashatu Kijaji amesema Serikali inaendelea kutekeleza Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara nchini (Blueprint) ili kuvutia uwekezaji na kuwezesha ufanyaji biashara wenye tija utaokuza uchumi wa taifa kwa ujumla.
Dkt. Kijaji ameyasema hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika anayeshughulikia Ukuzaji wa Uchumi na Taasisi kutoka Benki ya Dunia (WB),Dkt.Asad Alam na ujumbe wake kuhusu fursa za uwekezaji na ufanyaji biashara zilizopo Tanzania. 

Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi za Wizara jijini Dodoma leo Septemba 29, 2022.
Akiwa ameambata na viongozi wa Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara akiwemo Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Hashil Abdallah, Dkt. Kijaji amemhakikishia Mkurugenzi huyo kuwa Serikali iko tayari kushirikiana na Benki ya Dunia kuanzisha na kuendeleza programu mbalimbali za kuwawezesha wajasikiamaki wadogo na wa kati kuwekeza na kufanya biashara ili kukuza uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla.
Aidha, Dkt. Kijaji amesema Serikali inaendelea kufanya mamoresho mbalimbali kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara nchini ( Blueprint) ikiwemo kupitia na kurekebisha sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya Uwekezaji pamoja na kupunguza tozo mbalimba ambazo zimekuwa kikwazo katika ufanyaji biashara na uwekezaji.
Naye Mkurugenzi huyo wa Kikanda chini ya Benki ya Dunia amesema,Benki ya Dunia kupitia programu hiyo iko tayari kuwawezesha wajasirimali watanzania katika sekta mbalimbali kuendeleza biashara zao zitakazoongeza ajira, pato la Taifa na kuleta maendeleo ya kijamii na ya kiuchumi kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news