VIONGOZI WA KIJIJI, WANANCHI NA WAHANGA WA UJAMBAZI KATIKA KIJIJI CHA NYAMAKOBITI WILAYA YA SERENGETI MKOANI MARA WATUMA SALAMU KWA IJP WAMBURA

NA DIRAMAKINI

LEO Septemba 29, 2022 wakazi wa Kijiji cha Nyamakobiti kilichopo Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wametuma salamu za pongezi na asante kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IJP Camillius Wambura na jeshi lote la Polisi kwa operesheni mbalimbali za kutokomeza wahalifu kijijini hapo na maeneo mbalimbali nchini.
Wananchi hao wametuma salamu hizo kupitia mkutano wa hadhara wa wanakijiji ulioandaliwa na viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Nyamakobiti na maeneo ya jirani uliolenga kulipongeza Jeshi la Polisi na kuliomba liendelee na operesheni hizo za kudhibiti wahalifu kijijini hapo ili paendelee kuwa sehemu salama na wananchi waweze kufanya shughuli za kujiletea maendeleo bila hofu yoyote.
Aidha, wahanga wa vitendo vya uhalifu katika kijiji hicho wametoa shuhuda mbalimbali kueleza namna walivyoteswa na matukio ya ujambazi kwa kuibiwa mali zao kama vile mifugo, pikipiki pamoja na kujeruhiwa na kuuliwa na majambazi sugu kijijini hapo kabla ya Jeshi la Polisi kuwashugulikia kikamilifu.

Post a Comment

0 Comments