WAZIRI MKENDA AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI WA VENEZUELA MHE. YURI

NA MATHIAS CANAL-WEST

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda jana tarehe 5 Septemba 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Venezuela Mhe Yuri Pimentel anayeshughulikia maswala ya Afrika.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam na kujadiliana kwa kina kuhusu mambo mbalimbali ya ushirikiano kwenye elimu, sayansi na teknolojia.
Mara baada ya mazungumzo hayo Waziri Mkenda alishudhudia utiaji saini ya makubaliano kati ya Tanzania na Venezuela kwenye sekta mbalimbali ikiwemo elimu, sayansi na teknolojia uliofanywa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Mhe.Balozi Liberata Mulamula na Naibu Waziri huyo wa Venezuela Mhe Yuri Pimentel anayeshughulikia masuala ya Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news