NA DIRAMAKINI
SERIKALI ya Tanzania imetangaza msamaha wa kutokushitakiwa kwa mtu yeyote ambaye atasalimisha silaha anayoimiliki isivyohalali na kwamba usalimishaji huo utafanyika katika vituo vya Polisi, ofisi za serikali za mitaa au vijiji.
Pia mtu yeyote atakayepatikana na silaha haramu baada ya muda huo wa msamaha kupita atachukuliwa hatua kama mhalifu mwingine.

Akizungumza jijini Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa mwezi wa msamaha wa usalimishaji silaha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini amesema kuwa, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wataendesha kampeni maalum ambayo itashirikisha kamati za usalama za mikoa na wilaya, taasisi za kidini, vyombo vya habari na wadau wengine.

IJP Wambura amewataka pia wanaomiliki silaha kihalali kuzingatia sheria na kanuni zilizopo ili silaha hizo zisiangukie kwenye mikono ya wahalifu