Yanga SC yaichakaza Zalan FC mabao 4-0

NA DIRAMAKINI

BAADA ya dakika 45 za awali kutamatika katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya awali, Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam huku Zalan FC dhidi ya Yanga SC wakitoka bila bao.

Kipindi cha pili kimeanza kwa Yanga SC kupiga mpira wa nguvu ambao umewawezesha kuimiminia Zalan FC kutoka nchini Sudan mvua ya mabao.

Ikumbukwe kuwa, chini ya Kocha wa Yanga, Prof.Nasreddine Nabi alipokwenda mapumziko aliwapa mbinu mpya za kuibuka na ushindi.

Alianza Mayele dakika ya 47 kutupia bao ambalo liliwanyanyua mashabiki wa Yanga SC katika viti huku dakika ya 55 Feisal akitumbukiza bao la pili.

Mabao yaliyofuata ni ya Mayele ambapo hadi dakika tisini zinatamatika katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Yanga SC imejizolea alama tatu ikiwa na mabao manne

Post a Comment

0 Comments