Dangalo: Nimeamua kujiondoa baada ya kuona vichwa ni vilevile vilivyonipiga vibaya

NA DIRAMAKINI

EZEKIEL DANGALO ambaye ni mmoja kati ya wagombea wa nafasi ya uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Babati Vijijini mkoani Manyara ameamua kujitoa katika uchaguzi kwa madai ya kuwa na hofu ya kushindwa baada ya kushindwa katika uchaguzi wa awali.

Aidha, kwa mujibu wa Katiba ya CCM, mgombea haruhusiwi kujiondoa siku ya uchaguzi, hivyo wajumbe wanaweza wakaamua kumchagua ama wasimchague.
“Nimeamua kujiondoa baada ya kuona vichwa ni vilevile vilivyonipiga vibaya kwenye uchaguzi wa awali hivyo nimeogopa,”amesema Dangalo.

Hata hivyo, leo Oktoba 2,2022 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinafanya uchaguzi kuchagua viongozi katika ngazi za wilaya ambao wataongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Post a Comment

0 Comments