Dar kuyakutanisha mataifa 15 Jumanne

*Wasichana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 wana uwezekano mara tatu zaidi wa kupata VVU kuliko wavulana wa rika hilo katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara

NA GODFREY NNKO

OKTOBA 11 ambayo ni Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike, Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa (UN Women) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watakuwa wenyeji wa mkutano wa ngazi ya juu wa kutetea uongozi wa wanawake vijana kwa msaada wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR).

Mkutano huo utawaleta pamoja viongozi wanawake vijana wanaochipukia kutoka nchi 15 za Afrika ambapo wasichana wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi ya kuambukizwa VVU huku wakikutanishwa na mawaziri wanawake wa afya, elimu na usawa wa kijinsia.

Nchi washiriki itakuwa ni Botswana, Cameroon, Cote d’Ivoire, Eswatini, Kenya, Lesotho, Malawi, Mozambique, Namibia, Rwanda, South Africa, Tanzania, Uganda, Zambia na Zimbabwe.

PICHA NA MTANDAO.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Wanawake Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, mkutano huo utafanyika Oktoba 11, 2022, kuanzia saa 9:00-10:20 asubuhi katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam, Tanzania na vyombo vya habari vinaweza kuhudhuria kikao cha ufunguzi katika hoteli hiyo kuanzia saa 9:00-10:20 asubuhi ili kusikia maelekezo ya viongozi.

Viongozi mbalimbali wanatarajiwa kushiriki akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan, Mhe.Donald J. Wright, Balozi wa Marekani nchini Tanzania,Bi. Sima Bahous, Mkurugenzi Mtendaji, UN Women, Bi.Winnie Byanyima.

Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji, UNAIDS, 90+ viongozi wanawake vijana wenye umri wa miaka 18-24 (watakaojiunga na mtandao na ana kwa ana), mawaziri 35 wanawake na viongozi mashuhuri katika sekta ya afya, elimu na jinsia.

Mkutano huo wa viongozi wa wanawake wa ngazi mbalimbali, wa kisekta utafikia kilele kwa kutoa mapendekezo kwa watunga sera kuendeleza ili kusaidia kupunguza matukio ya VVU miongoni mwa wasichana balehe na wanawake vijana katika nchi zao.

Washirika wa ziada ni pamoja na Mtandao wa Viongozi wa Wanawake wa Afrika,Umoja wa Mataifa Tanzania, na Shirika la Kupambana na Ugonjwa wa Ukimwi la Umoja wa Mataifa (UNAIDS). Washiriki watajiunga ana kwa ana na mtandaoni.

"Kila baada ya dakika mbili msichana au mwanamke kijana aliambukizwa VVU Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika mwaka 2021. Mkutano huu wa ngazi ya juu ni sehemu ya mpango mpana unaoungwa mkono na UN Women na PEPFAR ili kutoa mafunzo ya uongozi na ushauri kwa vijana wa Kiafrika, wanawake ili waweze kutetea kwa mafanikio upatikanaji wa huduma za VVU bila ubaguzi na kuungana na watunga sera ili kuwa na sauti katika maisha yao ya baadaye,"imeeleza sehemu ya taarifa kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Wanawake ya Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news