HIZI HAPA BAADHI YA MALI ZITOKANAZO NA UHALIFU ZILIZOTAIFISHWA NA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA

Nyumba hii iliyopo kiwanja Na.210 Kitalu J kilichopo eneo la Mbezi Beach Dar es Salaam ilitaifishwa katika shauri la uhujumu uchumi namba 32 /2019 R v. John Hugo Kinyaki na mwenzake, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mbao hizi zilitaifishwa katika Shauri la Uhujumu Uchumi Na. 11/2021 lililohusu kosa la kukwepa kodi, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe.
Gari hili lilitaifishwa katika shauri la uhujumu uchumi namba 10/2020 jijini Mwanza.
Kiwanja namba 337 na 338 Kitalu LL kilichopo eneo la Kilimahewa, Manispaa ya Mtwara, kilitaifishwa katika shauri la uhujumu uchumi Mjini Mtwara.
Kiwanja namba 1408 na 1409 Kitalu B kilichopo eneo la Mtandi, Wilaya ya Masasi Mtwara, kilitaifishwa katika shauri la uhujumu uchumi namba 4/2019 Jamhuri dhidi ya Kelvin Rajabu Ungele na Mwenzake, Mahakama Kuu Mtwara.
Nyumba hii iliyopo katika kiwanja namba 781 Msasani Peninsular jijini Dar es Salaam imetaifishwa.
Nyumba hizi (two in one) zilizopo katika eneo la Kagando – Kaifo Manispaa ya Bukoba ilitaifishwa katika shauri la Uhujumu Uchumi na. 26/2021.

Post a Comment

0 Comments