Kinglion Kibaha Factory yatoa ofa ya pikipiki, maguta, mabati kupitia maonesho yanayoendelea Pwani

NA ROTARY HAULE
 
WAMILIKI wa Kiwanda cha Kinglion Kibaha Factory mkonai Pwani kinachojishughulisha na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo Bodaboda,Guta na Mabati kimewaomba wananchi kununua bidhaa za kiwanda hicho kwa kuwa zina ubora wa kiwango cha hali ya juu.
Meneja mauzo wa kiwanda hicho, John Maduka ametoa ombi hilo leo Oktoba 5, 2022 katika Maonesho ya Tatu ya Uwekezaji na Biashara yanayofanyika katika viwanja vya stendi ya zamani ya Mailimoja Kibaha Mjini.

Maduka,amesema kuwa, kiwanda chao kinazalisha bidhaa nyingi ikiwemo Bodaboda na kwamba bidhaa zote zinazalishwa kwa ubora na kila mwananchi anaweza kuzipata kwa bei nafuu.
Amesema kuwa, maonesho hayo yanasaidia kwa kiasi kikubwa kutangaza bidhaa zao huku akisema mwananchi anaweza kupata bodaboda,guta na bati kwa bei ya maonesho na kuwataka wachangamkie fursa hiyo.

Maduka ameongeza kuwa, katika maonesho hayo zipo pikipiki za kisasa ambazo zinauzwa kwa bei ya shilingi milioni 3.5 na nyingine zikiuzwa shilingi milioni 2.5 huku gurudumu la matairi matatu (Guta) likiuzwa kwa sh.milioni 5.7.
Ametaja bidhaa nyingine kuwa ni pamoja na bati za kisasa ambapo Geji 26 zinauzwa kwa sh.19000 kwa mita moja na Geji 30 ikiuzwa kwa sh.12,500 kwa mita moja huku Geji 28 ikiuzwa kwa sh .15,500.

"Mimi niwaombe Watanzania waje kwenye banda letu la Kinglion hapa Kibaha Mailimoja ili wapate bidhaa zetu kwa bei rahisi ambazo zinatengenezwa hapa nchini,"amesema Maduka

Maduka amesema, Tanzania kwa sasa kuna kila aina ya kiwanda na bidhaa nyingi zinazalishwa hapa nchini kwahiyo hakuna sababu ya kwenda nje kufuata bidhaa wakati Tanzania zipo.

Aidha,Maduka amefurahishwa na Serikali ya Mkoa wa Pwani kuweka maonesho hayo kwakuwa faida yake ni kubwa huku akiomba maonesho hayo yawe yanafanyika mara kwa mara katika mikoa mbalimbali.
"Tunaipongeza Serikali yetu ya Awamu ya Sita chini Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa jinsi ambavyo wamekuwa na jitihada za kuwasaidia wawekezaji kwani kwa sasa wapo huru katika uzalishaji,"amesema Maduka

Hata hivyo, maonesho ya wiki ya biashara na uwekezaji yameanza kufanyika leo Mjini Kibaha chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara nchini (TANTRADE) kwa ushirikiano wa Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) Kanda ya Mashariki na yatafikia kilele chake Oktoba 10,mwaka huu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news