Mama Mariam Mwinyi aushukuru Wakfu wa Health Rockfeller, kufanikisha chanjo ya UVIKO-19

NA DIRAMAKINI

MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mariam Mwinyi ameishukuru Jumuiya Health Rockfeller Foundation kutoka nchini Marekani kwa azma yake za kusaidia juhudi za Serikali katika kujikinga na Ugonjwa wa UVIKO-19.
Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) (kushoto) abadilishana mawazo na Makamu wa Rais wa Taasisi ya Rockfeller,Andrew Sweet mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation ZMBF iliyopo Migombani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. (Picha na Ikulu).

Mama Mariam ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) ametoa shukurani hizo Ikulu Migombani jijini Zanzibar baada ya mazungumzo na Ujumbe wa Jumuiya Health Rockfeller Foundation ulioongozwa na Makamu wa Rais Andrew Sweet, ambapo Jumuiya hiyo itasaidia Progamu ya utoaji wa chanjo za Ugonjwa wa UVIKO-19 hapa nchini.

Amesema, ZMBF inathamini juhudi za jumuiya hiyo kwa vile inalenga kuimarisha afya za wananchi katika kujikinga na ugonjwa huo.
Amesema, mradi huo ni wa mwaka mmoja na utatekelezwa kwa ushirikiano kati ya jumuiya hizo mbili, AMREF pamoja na Wizara ya Afya katika Wilaya za Magharibi ‘A’ pamoja Kaskazini ‘A’ Unguja .

Naye Makamo wa Rais wa Jumuiya ya Health Rockfeller Foundation Andrew Sweet amesema ni jambo la faraja kwa jumuiya hiyo kuwa na ushirikiano na ZMBF na kupata fursa ya kuwasaidia huduma za chanjo ili wananchi waweze kukabiliana na ugonjwa UVIKO-19.

Aidha, Mjumbe wa Bodi ya ZMBF, Dkt.Ellen Mkondya Senkoro amesema , programu inayolengwa kutekelezwa ni kubwa na kubainisha matumaini yake kuwa mradi huo utatoa matokeo chanya.

Post a Comment

0 Comments