Mawaziri wa Wizara za Kisekta watoa maagizo kwa viongozi wa mikoa, wilaya

NA MUNIR SHEMWETA, WANMM

NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Khamis Hamza Chillo amewataka viongozi wa mikoa na wilaya nchini kutoa elimu ya upandaji miti kwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Queen Sendiga akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Kamkolwe Kata ya Mpombwe Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Oktoba 11, 2022.(PICHA NA WIZARA YA ARDHI).
Mawaziri wa Wizara za Kisekta wakiwasili katika Kitongoji cha Kamkolwe Kata ya Mpombwe Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa walipotembelea kitongoni hicho Oktoba 11, 2022.

Aidha, ametaka viongozi hao kwenda kuelimisha wananchi namna bora ya kutunza vyanzo vya maji na kueleza kuwa changamoto kubwa iliyopo kwenye vyanzo hivyo ni shughuli kubwa za kibinadamu.
Naibu Waziri Chillo ametoa kauli hiyo mkoani Rukwa Oktoba 11, 2022 wakati wa ziara ya Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta kupeleka mrejesho wa Baraza la Mawaziri kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975.

Amesema, maeneo mengi yanayovamiwa wavamizi wake hawaendi tu kuvamia bali wanakata na miti na kuharibu vyanzo vya maji ambapo aliwataka viongozi wa mikoa na wilaya kuwaeleza wananchi ambao vijiji vyao vitabaki basi wapande miti.
"Watu waende kupata miti na si kupanda tu bali waishughulikie miti wanayoipanda,"amesema Chillo.

Akigeukia suala la utunzaji vyanzo vya maji, amesema mbali na uchafuzi wa mazingira unaofanywa wenye maeneo yaliyovamiwa, lakini wengine wanaharibu kabisa kwa kujenga nyumba na mwisho wa siku wanaharibu mazingira.
"Kikubwa sisi kazi tuliyokuwa nayo ni kwenda kuwaambia wananchi waende wakaheshimu na kutunza vyanzo vya maji na shughuli zetu za kibinadamu zisiharibu mazingira,"amesema Chillo.Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki aliwataka viongozi wa mikoa na wilaya kutekeleza na kumaliza kazi iliyo mbele ya kushughulikia changamoto za ardhi Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta iendelee na mambo mengine.

"Tusimsoneneshe rais kwa kuanzisha migogoro mingine maana atasikitika sana kwamba ametoa rasikimali fedha, watu na muda kumaliza migogoro halafu tuanzishe kamati nyingine na tujitahidi kuanzia ngazi ya chini ili kudhibiti migogoro inayoweza kutokea katika maeneo mengine,"amesema.Ridhiwani Kikwete ambaye ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amewataka watendaji wa sekta ya ardhi kuacha nidhamu ya woga kwa kutekeleza maelekezo ya wanasiasa bila kufuata taratibu.

"Wataalamu wetu waelekezeni viongozi wa siasa taratibu za kupata maeneo, mkituachia sisi tukioongoza harakati mwisho wa siku mnatengeneza hapa maeneo yote kuvamiwa na hakuna taratibu halafu mtakuja kusema walikuwa viongozi hawakufanya lolote kumbe wewe mwenyewe ni sehemu ya uvurugaji,"alisema Ridhiwani.
Kwa upande wake Naibu Waziri OR- TAMISEMI, David Silinde alisema ofisi yake kwa sasa haitasajili kijiji au maeneo ya utawala bila kushirikiana na wizara nyingine za kisekta kwa lengo la kujua kama maeneo hayo hayako kwenye hifadhi au eneo oevu sambamba na kupata mapendekezo ya mipaka kutoka wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi.

Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde aliwataka viongozi katika mikoa kuhakikisha kunakuwa na mipango ya matumizi bora ya ardhi hasa kupanga maeneo ya kilimo na wizara yake kwa sasa iko kwenye mchakato wa kutunga sheria ya kilimo ili kutunza maeneo yanayofaa kwa kilimo na kutumika kwa kazi hiyo.
"Hivi sasa tuna ushirikiano mzuri na wizara ya ardhi yale maeneo yote yanayobainika kufaa kwa kilimo tu nuyagazette ili kuwa na ulinzi wa maeneo hayo na mwisho wa siku pasiwepo tunataka pasiwepo muingiliano wa matumizi ya ardhi na tunaamini kupitia mkakati huu tutapunguza changamoto kubwa ya wakulima na wafugaji," alisema Mavunde.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja alieleza kuwa, changamoto kubwa katika uhifadhi ni muingiliano wa shughuli za binadamu na hifadhi na kuwaomba viongozi kushiriliana na kwa kusimamia kila mtu akasimamie eneo lake na kusisitiza kuwa wakifanya hivyo basi migogoro itaisha.

"Tukiwapa maelekezo ya kutosha na kusimamia hatutafika hapa tulipofika na hii jamani tukitoka humu kila mtu akielewa tiyokubaliana akatekeleze,"amesema Masanja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news