MBIBO AUNGA MKONO JUHUDI ZA STAMICO

*Shigella atoa Ofa kwa wawekezaji kumi wa mwanzo

NA MWANDISHI WETU

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo ameunga mkono jitihada zinazofanywa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa kununua mkaa mbadala unaotokana na makaa ya mawe unaotekelezwa na Shirika hilo.
Mbibo amenunua mkaa huo baada ya kushiriki katika Siku ya Geita iliyotanguliwa na kongamano la uwekezaji na baadaye kutembelea banda la STAMICO katika Maonesho ya 5 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini.

Aidha, Mbibo ametoa wito kwa STAMICO kuendelea kuutangaza mkaa huo ili wananchi waweze kuutambua na kuutumia kwa lengo la kuepusha ukataji wa miti na uharibifu wa mazingira.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigella amezindua Jarida maalumu linaloangazia fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo ndani ya mkoa wa Geita.

Sambamba na hayo, Shigella amewaomba wawekezaji kuchangamkia fursa zilizopo mkoani humo ambapo ametoa ofa kwa wawekezaji kumi wa mwanzo watapatiwa eneo la kuwekeza bila malipo.
Maonesho ya 5 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita yanatarajiwa kufungwa leo Oktoba 8, 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news