Waziri Dkt.Jafo atoa wito kwa STAMICO

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jafo amelitaka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuongeza uzalishaji na usambazaji wa mkaa mbadala unaotokana na makaa ya mawe.
Dkt. Jafo ameyasema hayo baada ya kutembelea Maonesho ya 5 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini 2022 yanayoendelea mkoani Geita.
Aidha, Dkt. Jafo ameipongeza STAMICO kwa kuja na ajenda ya matumizi ya mkaa rafiki kwa mazingira ambayo imeonesha kuwa mwarobaini wa matumizi ya mkaa utokanao na miti utakao punguza athari za mazingira.

Pia, Dkt. Jafo ametoa wito kwa wachimbaji wadogo wa madini na wadau wote wa madini nchini kutunza mazingira kwa lengo la kuepuka athari za mazingira.
Pamoja na mambo mengine, Dkt. Jafo amewataka wachimbaji wadogo wa madini na wadau wote wa madini kufika katika maonesho hayo ili kujifunza namna bora ya matumizi ya teknolojia ikiwemo matumizi ya chuma badala ya miti.

Katika hatua nyingine, Dkt. Jafo ameipongeza STAMICO kwa kuendelea kuwalea wachimbaji wadogo wa madini.
Jafo amesema matumizi ya miti kwa lengo la kukwepa gharama za matumizi ya chuma kuwa ni miongoni mwa sababu za uharibifu wa misitu unaofanywa na wachimbaji wadogo.
Miongoni mwa madhara hayo ni kupotea kwa uoto wa asili, ukame, kukauka kwa vyanzo vya maji, kukosa mapato yatokanayo na uhifadhi na mwishowe umaskini.

Post a Comment

0 Comments