NA SHAMIMU NYAKI
NAIBU Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Pauline Gekul ameipongeza timu ya Taifa ya Wanawake chini ya Miaka 17 (Serengeti Girls) kwa ushindi wa magoli mawili kwa Moja dhidi ya Ufaransa.
Mechi hiyo ya Kundi D iliyochezwa Oktoba 15, 2022 Uwanja wa Pandit Jawaharlal Nehru jijini Goa, India imeipandisha Tanzania hadi nafasi ya pili nyuma ya Japan na mbele ya Canada na Ufaransa katika kundi hilo.Kwa upande wake Kocha wa timu Bakari Shime, amesema vijana wanaendelea kuimarika na kusahihisha makosa ya Mechi ya kwanza dhidi ya Japan ambayo leo umeleta matokeo mazuri.

