'Mipango ya maendeleo inategemea kiwango cha ubora, ustadi, maarifa, utaalamu na uwajibikaji'

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dokta Hussein Ali Mwinyi, amekaribisha mashirikiano kati ya Serikali, Wawekezaji na Taasisi za Kitaalamu katika Usimamizi wa Miradi, ili kufanikisha mipango ya maendeleo, kwaajili ya kukuza Uchumi wa Nchi.
Dokta Mwinyi ameelekeza hayo Oktoba 20,2022 kupitia hotuba yake iliyosomwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, wakati wa Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka, wa Taasisi ya Kimataifa ya Uendeshaji wa Miradi (PMI) Tawi la Tanzania, huko Hoteli ya Golden Tulip, Uwanja wa Ndege, Mkoa wa Mjini-Magharibi Unguja.
 
Hivyo amesema Mpango wa Maendeleo wa 2025 na ule wa Dira ya Zanzibar ya Mwaka 2050, sambamba na Dira ya Maendeleo Ya Tanzania 2025, na ile ya 2050, kwa pamoja na kwa kiasi kikubwa, inategemea kiwango cha ubora, ustadi, maarifa, utaalamu na uwajibikaji, mambo ambayo yakikosekana, Taifa litashuhudia miradi mingi ya maendeleo ikishindwa kuleta tija, kinyume na matarajio, kutokana na kufeli usimamizi wake.

Post a Comment

0 Comments