Naibu Katibu Mkuu Mmuya atoa rai kwa watendaji wa Serikali

NA MWANDISHI WETU

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Bw.Kaspar Mmuya ametoa rai kwa watendaji wa Serikali kutunza vizuri vyombo vya usafiri walivyopewa ili viweze kuwasaidia katika utendaji wa kazi na kudumu kwa muda mrefu.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Bw.Kaspar Mmuya akizungumza na watendaji wa Ofisi ya Mpigachapa jijini Dar es Salaam.

Wito huo umetolewa wakati wa kukabidhi bajaji mbili kwa watumishi wa Ofisi ya Mpiga Chapa wa Serikali jijini Dar es Saalam katika kuwajengea mazingira mazuri watu wenye ulemavu ya utendaji wa kazi.
“Ofisi ya Waziri Mkuu moja ya jukumu lake ni kuwezesha watu wenye ulemavu kwa kusimamia Sera ya Watu wenye Ulemavu na Miongozo ya watu wenye Ulemavu,”amesema.

Akitoa neno la shukrani, Bw.Ophin Malley ameshukuru Serikali kwa kuwatambua watu wenye ulemavu katika mazingira waliyonayo mahala pa kazi.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu,Bw. Kaspar Mmuya akikabidhi funguo kwa watendaji wa Ofisi ya Mpiga Chapa.

“Tunaomba kama itafaa tuweze kupatiwa baiskeli maalumu ili zituwezeshe kuturahisishia kutoka sehemu moja kwenda nyingine wakati wa utendaji wa kazi,”amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news