Ndoro achaguliwa Mwenyekiti CCM wilayani Ruangwa

NA MWANDISHI WETU

WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa CCM wilayani Ruangwa mkoani Lindi kutoka kata 22 wamemchagua, Ibrahim Issa Ndoro kuwa Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Mwnyekiti wa CCM wa wilaya ya Ruangwa, Ibrahim Issa Ndoro baada ya Mwenyekiti huyo kuibuka mshindi katika Mkutano Mkuu wa CCM wilaya ya Ruangwa wa Uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Awali na Msingi, Wonder Kids, Oktoba 2, 2022. Ndoro alijizolea kura 921 na kuwabwaga washindani wake, Rashid Nakumbya aliyepata kua 21 na Fatuma Rashidi Ng’ombo aliyepata kura 17. Jumla ya kura zilizopigwa zilikuwa 966, kura 7 ziliharibika. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Katika Mkutano huo ambao uliofanyika Oktoba 2, 2022 na kuhudhuriwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Kassim Majaliwa.

Ndugu Ndaro aliibuka mshindi katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Awali na Msingi, Wonder Kids.

Ndoro alijizolea kura 921 na kuwabwaga washindani wake, Rashid Nakumbya aliyepata kura 21 na Fatuma Rashidi Ng'ombo aliyepata kura 17. Jumla ya kura zilizopigwa zilikuwa 966, kura 7 ziliharibika.

Akizungumza na wajumbe wa mkutano huo Ndugu Ndaro ameahidi kuendeleza na kuimarisha uhusiano kwa WanaCCM katika wilaya ya Ruangwa "Ninawashukuru sana ndugu wajumbe kwa imani yenu kwangu, kwa kuona ninafaa kuwaongoza katika wilaya hii, ninawaahidi ushirikiano na kufanya kazi iliyotukuka kwa ajili ya chama chetu"

Aidha katika uchaguzi huo, Msimamizi wa uchaguzi Shaibu Ndemanga aliwatangaza Ndugu Ramadhani Ibrahim Matola aliyepata kura 663, Julius Charles Mukheben aliyepata kura 640 na Hassan Twaha Ngoma ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa aliyepata kura 557 kuwa washindi wa nafasi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa.

Pia Ndugu Kasambe Hokororo alichaguliwa kuwa Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news