Rais Dkt.Mwinyi afanya uteuzi leo, Bihindi kupangiwa kazi nyingine

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo Oktoba 3, 2022 amefanya uteuzi.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena A.Said.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Omar Ali Yussuf kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) katika Wizara ya Maji, Nishati na Madini.

Uteuzi wa Omar unaanza leo ambapo awali alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA).

Aidha, kwa mujibu wa taarifa hiyo,ndugu Bihindi Nassor Khatib aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) atapangiwa kazo nyingine.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news