Onesho la Kimataifa la Utalii la Swahili (S!TE) ni fursa Dar es Salaam-Mheshimiwa Masanja

NA HAPPINESS SHAYO-WMU

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Masanja (Mb) amesema, uwepo Onesho la Kimataifa la Utalii la Swahili (S!TE) katika Jiji la Dar es Salaam ni fursa kubwa kwa jiji hilo kutangaza vivutio vyake.
Amesema kuwa, Jiji la Dar es Salaam ndio lango Kuu la Biashara Tanzania na kwamba wageni wengi wanaofika nchini wanafikia katika Jiji hilo na kisha kuelekea kwenye maeneo mengine ya utalii.

Mhe.Masanja ameyasema hayo alipozungumza na waandishi wa habari Oktoba 21,2022 wakati wa mahojiano maalum yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam linapofanyika Onesho la S!TE 2022.
Aidha, ameeleza kuwa Jiji la Dar es Salaam lina historia ya kipekee kutokana na vivutio vilivyopo vya kiutamaduni ikiwemo majengo na malikale.
“Jiji la Dar es Salaam lina historia kubwa na nzuri ya kiutalii kutokana na uasilia wake. Kuna maeneo mengi ya kiutalii ikiwemo majengo na malikale hivyo Onesho hili litafungua fursa za kiutalii katika Jiji hili,”amesema Mhe. Masanja.
Akizungumzia onesho hilo linalotarajia kumalizika rasmi Oktoba 23, 2022, Naibu Waziri huyo amesema lengo kuu la onesho hilo ni kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko nchini Tanzania, na kukutanisha wanunuzi na wauzaji wa bidhaa za utalii wa Kitaifa na Kimataifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news