Polisi awatandika wenzake risasi Kenya, aua naye ajitandika

NA DIRAMAKINI

AFISA wa Jeshi la Polisi nchini Kenya leo Oktoba 23,2022 amejiua kwa risasi dakika chache baada ya kuwapiga risasi wenzake wawili katika Kituo cha Polisi cha Moyale, Kaunti ya Marsabit.

Maafisa kutoka DCI wakitazama eneo husika.(Picha na Kenyans.co.ke).

Kaunti hiyo ni miongoni mwa kaunti chache nchini Kenya ambazo zimekuwa zikikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa usalama,hivi karibuni Kenya ilipeleka maelfu ya polisi na maafisa wengine wa usalama katika eneo hilo kufuatia kuzuka kwa ghasia za kikabila.

Serikali ilisema ukame, uchochezi wa kisiasa na kuwepo silaha kutoka nchi jirani ya Ethiopia ni miongoni mwa sababu ambazo zinastahili kulaumiwa kwa kudorora kwa hali ya usalama kwenye eneo la mpakani.

Pia, wizi wa ng’ombe umeongezeka sana huko Marsabit ambayo ni moja ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi na ukame kote katika Pembe ya Afrika.

Sasa, turejee katika kisa cha askari polisi kujiua leo. Kwa mujibu wa ripoti ya polisi iliyoonwa na wavuti ya Kenyans imeeleza kuwa, afisa huyo aliiba bunduki hiyo kutoka kwa mwenzake kabla ya kuelekea kwenye hifadhi ya silaha ambapo aliwaua polisi wengine wawili.

"PC Lawrence alichukua jiwe kubwa na kumpiga PC Orero kwenye paji la uso akachukua bunduki yake kabla ya kukimbilia kwenye ghala la silaha ambapo maafisa wengine walikuwa wakichukua silaha kwa kazi ya siku hiyo.

"Alipiga risasi katika safu ya wasimamizi, na kumuua papo hapo na pia kumfyatulia risasi PC Matete,"imeeleza sehemu ya ripoti hiyo.

Aidha, Afisa wa tatu alipata jeraha la risasi katika mkono wake wa kushoto. Kisha afisa huyo alirudi nyumbani kwake, ambako alijichomoa.

"PC Kumber kisha akarudi nyumbani kwake ambapo alifunga mlango kwa ndani na kujipiga risasi kidevuni," ilisomeka taarifa hiyo kulingana na kitabu cha matukio (OB Namba 09/23/10/2023).

Miili ya marehemu imesafirishwa hadi katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya kaunti ndogo ya Moyale. Huku, maafisa wawili waliojeruhiwa wakikimbizwa katika Hospitali ya Alhilal. Kulingana na polisi, askari aliyepigwa risasi mikononi mwake yuko katika hali mbaya.

Wakati huo huo, Kamishna wa Kaunti ya Moyale Paul Rotich amevieleza vyombo vya habari kuwa, sababu ya shambulio hilo bado haijajulikana. Hata hivyo, maafisa wameanzisha uchunguzi kuhusu suala hilo.

Tukio hilo la mapema asubuhi linajiri huku kukiwa na wasiwasi kutokana na kuongezeka kwa visa vya kujitoa uhai na mauaji miongoni mwa maafisa wa polisi nchini humo.

Hata hivyo, wakati wa kuhakikiwa na Bunge la Kitaifa, Waziri wa Mambo ya Ndani aliyeteuliwa Kithure Kindiki aliahidi kushughulikia ustawi wa maafisa waliovalia sare ikiwa ni pamoja na hali yao ya kiakili.

"Ikiidhinishwa, ninanuia kuandaa, kupanua na kutumia kikamilifu vitengo vya afya na ushauri, ambavyo vitaunganishwa na Huduma ya Polisi ya Kenya na hospitali za Huduma ya Magereza," alisema Kindiki.

Post a Comment

0 Comments