RAIS RUTO KUWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MBILI

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Dkt. William Samoei Ruto anatarajiwa kuwasili nchini leo jioni kwa ziara ya kikazi ya siku mbili(tarehe 09-10, Oktoba 2022).

Picha na Getty Images.

Mhe. Dkt. Ruto na Ujumbe wake akiwemo mke wake Mama Rachel Ruto utakapowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere utapokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mhe. Dkt. Stergomena Tax.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Mambo na Ushirikiano wa Afrika Mashariki leo imefafanua kuwa, tarehe 10 Oktoba 2022, Mhe. Dkt. Ruto atawasili Ikulu ya Dar es salaam na kupokelewa na Mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan.

Rais Ruto pamoja na mambo mengine, atashiriki mazungumzo rasmi na Mwenyeji wake Mhe. Samia Suluhu Hassan na baadaye kuzungumza na waandishi wa habari kabla ya kushiriki dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima yake na Rais Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Dkt. Ruto na ujumbe wake wanatarajiwa kuondoka nchini kurejea Kenya baada ya kukamilika kwa dhifa ya kitaifa

Post a Comment

0 Comments